April 21, 2015


Majeruhi mfululizo yanaonekana kumchanganya Kocha Hans van der Pluijm.



Pluijm anaonekana kuchanganyikiwa kwa kuwa ndiyo kipindi muhimu kwa kikosi chake cha Yanga kupigania kutwaa ubingwa lakini kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi ya marudiano dhidi ya Etoile ya Tunisia.

Kelvin Yondani, Salum Telela na nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro', wote ni majeruhi.

"Inachanganya kwa kiasi kikubwa. Mechi za mwisho za ligi ni muhimu kwa ajili ya kutwaa ubingwa lakini unakosa wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza.

"Inachanganya lakini lazima kuwe na namna ya kujua na kufanya kila linalowezekana ili tufanye vema.

"Daktari anaendelea kushughulikia maumivu yao, tunaamini watakuwa vizuri ndani ya siku chache wakati sisi tukiendelea kupambana," alisema Pluijm.

Yanga inashinda dimbani kucheza na Stand United ya Shinyanga. Inahitaji mechi tatu tu kutwaa ubingwa.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic