Suala la mrembo anayedaiwa kuwa mpenzi wa kipa
Peter Manyika limeendelea kutajwa kuwa ndiyo sababu ya kushuka kwa kiwango
chake.
Kocha wa Simba, Goran Kopunovic amemteremsha
Manyika kucheza kikosi cha pili ili kuinua kiwango chake.
Lakini taarifa za ndani kutoka Simba zimeeleza
mrembo huyo aitwaye Naima maarufu kama Nimaa ndiyo chanzo cha kuporomoka kwa
kiwango.
“Hivi karibuni alisema asifuatwefuatwe, Manyika
anaona kama anaonewa watu kumueleza kuhusu huyo mpenzi wake.
“Lakini kocha analalamika kuwa ameonyesha
kiwango cha chini katika mechi zilizopota. Lakini yeye ni mbishi sana,”
kilieleza chanzo.
Mara ya kwanza baada ya kunaswa na mrembo huyo,
Manyika alikanusha na kudai Nimaa ni rafiki yake tu.
Lakini kwa sasa hali ilivyo, wawili hao wamekuwa
wakijiachia hadharani na kuachana na mambo ya woga.
0 COMMENTS:
Post a Comment