July 1, 2015

NGOMA (KUSHOTO) AKITETA JAMBO NA SALEH ALLY 'JEMBE' (KULIA). KATIKATI NI ZUTTAH AKIINGIA KWENYE GARI.
Mshambuliaji Donald Ngoma amerejea kwao Zimbabwe kwa ajili ya maandalizi ya siku chache kabla ya kurejea nchini kujiunga rasmi na Yanga.

Ngoma ameiambia SALEHJEMBE kwamba atarejea nchini Jumapili na Jumatatu ataanza kazi rasmi na timu yake mpya.

Mzimbabwe huyo amesema ameomba ruhusa ya siku nne kwa kuwa alikuwa amesafiri kwenda DR Congo kwa ajili ya sherehe fupi ya kuchumbia.
SALEH ALLY 'JEMBE' AKIWAAGA ZUTTAH NA NGOMA...

“Sasa sikuwa nimefanya maandalizi ya kutosha. Sasa narejea nyumbani, halafu Jumapili nitakuwa hapa. Nashukuru uongozi wa Yanga kwa kunisikiliza,” alisema.

Lakini kiungo kiraka Joseph Zuttah “Tetteh” raia wa Ghana yeye anaendelea kubaki nchini na tayari ameanza kazi na Yanga.

Wawili hao wamejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic