July 29, 2015

NIYONZIMA, HERMAN NGOMA NA MIGI.
Moja ya raha ya mechi ya leo ya robo fainali ya Kombe la Kagame kati ya Yanga dhidi ya Azam FC ni wale viungo wawili wa timu ya taifa ya Rwanda.


Haruna Niyonzima anaykipiga na Yanga na Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’ ambaye ametua Azam FC na michuano ya Kagame ni yake ya kwanza kuitumikia timu hiyo ya Chamazi, Dar es Salaam.
NIYONZIMA NA MIGI
Wawili hao, wote wamekulia kisoka katika timu ya APR ya Rwanda ambayo tayari imeng'olewa na kuvuliwa ubingwa na Al Khartoum ya Sudan.

Lakini wamekuwa wakikutana katika kikosi cha timu ya taifa, Niyonzima akiwa kiungo mchezeshaji na Migi akiwa kiungo mkabaji.

Kwa mifumo ya timu zao, maana yake, Migi atakuwa akifanya kazi ya kumkaba Niyonzima ambaye kikazi ni kaka yake.

Wanyarwanda hao wanafahamiana vizuri kikazi, kila mmoja anajua ubora wa mwenzake na madhara yake akipewa nafasi.

Wote wana uwezo wa kufunga, Niyonzima ni kupiga mashuti ya mbali na hatari kwa ile mipira ya kugongeana.

Hali kadhalika, Migi ni mzuri kwa mashuti lakini ana uwezo wa kupiga mipira ya vichwa akiutumia urefu wake.

Pia ni bora katika ukabaji na kama Kocha Stewart Hall atampa nafasi ya kwenda mbele, basi anaweza kuidhuru Yanga kwa kuwa ni mfungaji mzuri katika mechi kubwa.

Kama unakumbuka, Migi ndiye aliyeing'oa Simba katika michuano ya Kagame mwaka 2010 baada ya kufunga bao la ushindi na kuiacha Msimbazi ikilala kwa mabao 2-1.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic