July 29, 2015


Winga wa zamani wa Yanga na Azam FC, Mrisho Ngassa, amesema anawapa Wanajangwani nafasi kubwa kusonga mbele kwenye Kombe la Kagame ila amewaonya wachezaji wa kikosi hicho kucheza kitimu, siyo papara ya kila mmoja kutaka kufunga bao.


Leo Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga na Azam zinapambana katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Kagame, mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani wa hali ya juu.
Ngassa akizungumza kutoka Afrika Kusini anakocheza katika Klabu ya Free State Stars, alisema katika mchezo huo, Yanga ina nafasi ya kufanya vizuri kama wachezaji watacheza kwa kufuata maelekezo ya Kocha Hans van Der Pluijm muda wote.

Alisema wachezaji hao wakishirikiana vizuri huku wakipata hamasa kubwa kutoka kwa mashabiki wao, hiyo itakuwa ni tiketi yao ya kuweza kusonga mbele katika michuano hiyo ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati.

“Naitakia kila kheri Yanga, naamini itavuka hatua hiyo ya robo fainali ila wacheze kama timu na tatizo lipo pale kila mchezaji atakapotaka kucheza kivyake ili afunge.


“Watulie na kujipanga kwani Azam siyo timu mbaya, imeimarika sana siku hizi, hivyo wachezaji wa Yanga watulie na kufuata maelekezo ya kocha hakika watashinda,” alisema Ngassa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic