Kiungo wa zamani wa Stand United ya
Shinyanga, Charles Mishetto ametoa pasi mbili za bao 'asisti' katika mechi ya kirafiki
akiichezea timu yake nchini Ujerumani.
Misetto amesema walikuwa katika
maandalizi ya mwisho kabla ya ligi kuanza. Mishetto anakipiga katika kikosi cha Rabestein FC kinachoshiriki Ligi Daraja la Nne nchini Ujerumani.
“Ligi inaanza Agosti 8, hivyo tuko
katika maandalizi ya mwisho na tunapambana kweli.
“Ilikuwa mechi nzuri na tumeshinda
mabao matatu. Nilicheza dakika zote tisini. Kocha alinipanga namba sana,
nikatoa krosi mbili za mabao,” alisema Mishetto.
0 COMMENTS:
Post a Comment