August 28, 2015

KOUYATE NA FANNY...

Baada ya ukimya, mwanamitindo Fanny Naguesha sasa inaelezwa ameingia kwenye uhusiana wa kimapenzi na beki wa West Ham United, Cheikhou Kouyate.


Naguesha raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Nigeria alikuwa mpenzi wa Mario Balotelli, lakini wakazozana na kauchana miezi michache iliyopita.

Lakini Fanny ameanza kuonekana akiwa amevaa jezi za West Ham na mara nyingine akiwa na Kouyate huku akitupia maneno “rafiki bora daima”.

KOUYATE KAZINI

Mambo hayo yameanza kutafsiriwa kwamba taratibu anaingia kwenye uhusiano na Kouyate ambaye ni kitasa wa West Ham United .  

Hata hivyo kumekuwa na taarifa nyingine kwamba wawili hao wamekuwa marafiki wa karibu kwa kipindi kirefu na huenda hakuna uhusiano wa kimapenzi.



WAKATI AKIWA NA BALOTELLI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic