August 28, 2015


Mwanariadha nyota duniani, Usain Bolt amekubali kumsamehe mwandishi wa habari aliyemgonga na wote wakaanguka.


Mwandishi huyo alimgonga Bolt na kumwangusha wakati akishangilia mara tu baada ya kushinda mita 200 katika mashindano ya IAAF kwenye Uwanja wa Bird Nest jijini Beijing, China.

Bolt alikuwa anashangilia, mwandishi huyo alikuwa akimchukua kwa nyuma yake, ghafla akashindwa kukithibiti chombo cha Sagway alichokuwa amepanda, kikamchota Bolt, wote wakaanguka.

Lakini mwandishi huyo alitoa mkufu na kumpa Bolt akionyesha kumuomba msamaha kwa kilichotokea wakati yeye akichukua picha za TV.

Bolt naye kiroho safi kabisa akakubali zawadi hiyo na kumueleza alishamsamehe.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic