August 29, 2015


Kiungo mkabaji wa zamani wa Yanga sasa hivi Mwadui FC, Athumani Idd ‘Chuji’ ameanza vibaya na timu hiyo inayojiandaa na Ligi Kuu Bara baada ya kupata maumivu ya nyama za paja.

Chuji, kiungo aliyeipandisha daraja timu hiyo, alipata maumivu hayo kwenye mazoezi ya Mwadui ilipokuwa ikijiandaa na msimu ujao wa ligi kuu utakaoanza Septemba 12, mwaka huu.

Kiungo huyo, tayari amekosa michezo mitatu ya kirafiki dhidi ya Simba uliyochezwa Uwanja wa Taifa Dar, Azam FC (Azam Complex) na Friends Rangers (Uwanja wa Mwalimu Nyerere).

Akizungumzia majeraha hayo, Chuji alisema: “Naendelea vizuri lakini kwa mujibu wa madaktari walionifanyia vipimo wamenitaka nianze mazoezi baada ya wiki mbili kwa kuanza mazoezi mepesi ya binafsi kabla ya kujiunga na wenzangu, ninaamini kabla ya ligi kuanza nitakuwa tayari nimepona.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic