MAGURI AKIPAMBANA NA YONDANI NA CANNAVARO AMBAO WANAAMINIKA MABEKI IMARA ZAIDI WA KATI NCHINI. |
Baada hivi karibuni uongozi wa Simba kutangaza
kuachana na aliyekuwa mshambuliaji wake, Elias Maguri mambo yamebadilika
klabuni hapo na sasa inadaiwa viongozi wanahangaika kuhakikisha wanamrudisha
straika huyo mbishi.
Inadaiwa kuwa uongozi huo umefikia hatua hiyo
baada ya kutovutiwa na viwango vya washambuliaji wao wapya raia wa Senegal
waliotua klabuni hapo siku chache zilizopita kwa ajili ya majaribio.
Hivi karibuni uongozi huo ulishindwa kumvumilia
msambuliaji wake, Papa Niang aliyetua klabu hapo akitokea Senegal na tayari
umeshamfungashia virago, huku ikimleta Msenegal mwingine, Pape Abdoulaye kwa
ajili ya majaribio.
Simba baada ya kucheza mechi ya kirafiki na
Mwadui na kujikuta ikishindwa kufunga bao hata la kuotea ilijikuta ikijilaumu
kwa nini ilimuacha nyota huyo ambaye wanaamini kama angekuwepo basi angecheka
na nyavu.
Maguri alisema alipigiwa simu na baadhi ya
viongozi wa timu hiyo baada ya mechi dhidi ya Mwadui wakimwambia kuwa wanajuta
kwa uamuzi wao wa kumtimua kwani bado alikuwa muhimu kikosini hapo.
“Siwezi kuwataja majina yao lakini ukweli ndiyo
huo na waliambia kuwa ni bora wanirudishe kundini lakini niliwakatilia na
kuwaambia kuwa tayari nimeshaingia mkataba na Stand United hivyo kwa sasa
siwezi kurudi tena,” alisema Maguri.
0 COMMENTS:
Post a Comment