August 29, 2015

MAGURI AKIPAMBANA NA YONDANI NA CANNAVARO AMBAO WANAAMINIKA MABEKI IMARA ZAIDI WA KATI NCHINI.
Baada hivi karibuni uongozi wa Simba kutangaza kuachana na aliyekuwa mshambuliaji wake, Elias Maguri mambo yamebadilika klabuni hapo na sasa inadaiwa viongozi wanahangaika kuhakikisha wanamrudisha straika huyo mbishi.

Inadaiwa kuwa uongozi huo umefikia hatua hiyo baada ya kutovutiwa na viwango vya washambuliaji wao wapya raia wa Senegal waliotua klabuni hapo siku chache zilizopita kwa ajili ya majaribio.

Hivi karibuni uongozi huo ulishindwa kumvumilia msambuliaji wake, Papa Niang aliyetua klabu hapo akitokea Senegal na tayari umeshamfungashia virago, huku ikimleta Msenegal mwingine, Pape Abdoulaye kwa ajili ya majaribio.

Simba baada ya kucheza mechi ya kirafiki na Mwadui na kujikuta ikishindwa kufunga bao hata la kuotea ilijikuta ikijilaumu kwa nini ilimuacha nyota huyo ambaye wanaamini kama angekuwepo basi angecheka na nyavu.

Maguri alisema alipigiwa simu na baadhi ya viongozi wa timu hiyo baada ya mechi dhidi ya Mwadui wakimwambia kuwa wanajuta kwa uamuzi wao wa kumtimua kwani bado alikuwa muhimu kikosini hapo.


“Siwezi kuwataja majina yao lakini ukweli ndiyo huo na waliambia kuwa ni bora wanirudishe kundini lakini niliwakatilia na kuwaambia kuwa tayari nimeshaingia mkataba na Stand United hivyo kwa sasa siwezi kurudi tena,” alisema Maguri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic