Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema kuondoka kwa kocha
wao wa viungo kulikuwa kinajulikana.
Dusan Mormcilovic
ameondoka nchini huku akisema Yanga itaifunga Simba.
“Unajua hili suala
mnalikuza tu, Dusan alikuwa na mkataba wa miezi mitatu tu kwa ajili ya
pre-season. Alipomaliza akaondoka.
“Mfano tiketi yake
tokea amefika alikuwa anajua anaondoka jana, hivyo hakukuwa na kipya. Kwa sasa
tumemalizana na mambo maandalizi ya mwanzo wa msimu.
“Ikiwa tutamhitaji,
tutamuita tena. Hivyo hakuna ugomvi wala tatizo. Amekwenda kwao,” alisema Hans
Pope.
“Maandalizi mengine
yanaendelea kama kawaida na kila kitu kinakwenda vizuri. Hapa lengo ni kuwapa
ndugu zetu hawa supu ya miiba.”
0 COMMENTS:
Post a Comment