MALINZI |
Rais wa Shrikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
ametuma salam za rambirambi kwa Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry
kufuatia vifo vya mahujaji zaidi ya 700 vilivyotokea Maka wakati wa kuhiji.
Katika salam zake kwenda kwa mufti mkuu, Malinzi amewapa pole
waislam wote duniani kufuatia vifo vya mahujaji hao zaidi ya 700 vilivyotokea
juzi na majeruhi zaidi ya 400 wakati wa ibada ya hija.
Malinzi
amesema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini TFF inawapa pole wafiwa
wote, ndugu jamaa na marafiki na kuwatakia majeruhi afya njema na kusema ipo
pamoja nao katika kipindi hichi kigumu cha maombelezo.
0 COMMENTS:
Post a Comment