HII NDIYO SIRI YA MABAO YA OKWI NA KAGERE
KOCHA Mkuu wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems amesema kuwa mabao wanayoendelea kufunga washambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi na Mnyarwanda, Meddie Kagere ni sehemu ya ahadi waliyoitoa kwake baada ya kikao alichofanya nao.
Aussems amefurahishwa na safu hiyo ya ushambuliaji iliyocheza vizuri kwa kuelewana huku ikifuata maelekezo aliyowapa kabla ya mchezo.
“Nimewaambia wachezaji wangu wote wakiwemo washambuliaji akina Okwi, Kagere kuwa ninahitaji ushindi wa mabao mengi katika michezo iliyobaki ya ligi.
“Hivyo, ninafurahia kuona wachezaji wangu kadiri siku zinavyokwenda wanacheza kwa kubadilika wakifuata maelekezo yangu ninayowapa mazoezini nina matarajio makubwa ya kuwaona wakiendelea kubadilika kwa kufunga mabao mengi zaidi,”alisema Aussems ambaye bado Simba hawajampa mkataba mpya.
kama wanabadilika kwa jinsi unavyowaelekeza maana yake tutegemee ukame zaidi, maana walifunga goli sita then umefuata ukame vs Kagera na Ukame vs Azam
ReplyDeleteyupo kocha alituelekeza siri ya mfungaji ni UCHOYO, nina wasiwasi mwalimu amewaambia waache uchoyo ndio maana hawafungi