Mambo sasa yanaonekana si mazuri tena kwa ule
mfumo wa 4-4-2 ambao amekuwa akiuamini sana Kocha Diego Simeone.
Amekuwa akipoteza mechi mfululizo, jambo ambalo
tayari limezua mjadala mkubwa.
Wadau sasa wanamshauri Simeone kutumia mfumo wa
4-3-3 ambao unaweza kubadilisha mambo.
Mara kadhaa amekuwa akishauriwa katika hilo,
lakini raia huyo wa Argentina amekuwa akisisitiza kutumia 4-4-2.
Lakini kupoteza mechi mfululizo, kupotea kwa
ushindani kutoka katika kikosi chake kunaonekana kumlazimisha kubadili mfumo
huo na kuhamia 4-3-3 ambayo inakuwa na washambuliaji watatu mbele.
0 COMMENTS:
Post a Comment