VITA YAENDELEA TFF, KUULI AMVAA TENA KIDAO 'HUNA MAMLAKA'
Baada ya kuandikiwa barua ya kujieleza kwanini amesimamisha mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Simba, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Wakili Revocatus Kuuli amemwambia Katibu Mkuu TFF, Wilfred Kidao, kuwa hana mamlaka ya kumuingilia.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya Kuuli kuusimamisha mchakato wa uchaguzi Simba uliopo kwenye hatua ya uwasilishwaji wa mapingamizi kupitia wagombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Kuuli amesema kuwa yeye si mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF na hana mamlaka ya kupiga kumzuia kufanya maamuzi yake kwa sababu kamati hiyo ni huru.
Aisha Kuuli ameeleza kuwa Kidao ameingilia kamati ya uchaguzi iliyo huru na sasa anataka kuifanya ionekane kuwa si huru huku akieleza kuwa hawezi kumjibu chochote licha ya kutoa siku tatu.
Mwenyekiti huyo aliusimamisha mchakato wa uchaguzi Simba kwa muda baada ya mambo kadhaa kwenda kinyume na taratibu ikiwemo ada ya kugombea nafasi ya Uenyekiti na Ujumbe kuwa tofauti na ile ya wanachama wa TFF.
Simba wasipokuwa makini mgogoro utazuka mkubwa sana upande wao..
ReplyDeleteWataishia kwenye vyesi na mapingamizi ya kudumu..
Ushiriki wao TPL utakuwa wa kusua sua..!!
nimeshazungumzs kuwa hizi ni hujuma za wazi wanazofanyiwa Simba.Viongozi mnapaswa kukutana dharura na kuidhibiti hali hii ya mkanganyiko ndani ya TFF.Walianza kucheza na saikolojia za wachezaji walioitwa Stars kuwa hawana nifhamu na uzalendo.Wachezaji hawo iliwanyongonyesha kisakolojia.Sasa TFF wanapiga ngoma ili wanachama wa Simba waingie waicheze.Na matokeo yake ni vurugu ambazo hatutajua nani mpigaji ngoma na ninani anayeicheza.
ReplyDeleteHII SIO BURE. VIONGOZI SIMBA ANGALIENI KUNA HUJUMA ZINAANDALIWA. TUSIPOKUWA MAKINI, MGOGORO UNAOANDALIWA UTATUVURUGA NA TIMU ITAHARIBIKA NIA YAO UBINGWA TUUPOTEZE. VIONGOZI MUWE MAKINI.
ReplyDelete