Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm amesema wala hana
sababu ya kuwa na hofu kutokana na kumkosa Emmanuel Okwi.
Pluijm amesema hafanyi kazi kwa kuangalia majina makubwa na
badala yake mchezaji gani anayejituma mazoezini.
“Akikosekana Okwi huwezi kusema Yanga haiwezi
kucheza, tumeshinda mechi kadhaa bila ya kuwa na Okwi au wachezaji wengine.
“Yanga ni timu, haiwezi kuwa inamtegemea mtu
mmoja ndiyo maana nimesisitiza sipendi kumzungumzia sana,” alisema.
Okwi ameendelea na mgomo wake wa kususia kuichezea Yanga kwa kuwa anadai dola 40,000 zake za usajili.
Awali kulikuwa na mazungumzo kati yake na uongozi wa Yanga, lakini ghafla mambo yakawa kimya.
Okwi ameendelea na mgomo wake wa kususia kuichezea Yanga kwa kuwa anadai dola 40,000 zake za usajili.
Awali kulikuwa na mazungumzo kati yake na uongozi wa Yanga, lakini ghafla mambo yakawa kimya.
0 COMMENTS:
Post a Comment