KLABU ya Yanga imeibua upya utata mwingine wa mkataba wa mshambuliaji Bernard Morrison wakidai hana mkataba halali na mabosi wake wa sasa ambao ni Simba.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela amesema hayo leo Oktoba Mosi kwa kueleza kuwa wakati klabu yao ikipokonywa haki ya umiliki wa Morrison wamebaini mapungufu makubwa katika mkataba wa mchezaji huyo na Simba.
Mwakalebela ambaye amekuja na nakala anayodai ni ya mkataba huo amesema sehemu zote za mkataba huo zimesainiwa na mchezaji huyo pekee hatua ambayo sio sahihi.
Amesema katika mkataba huo pia hauna sehemu iliyosainiwa na kiongozi yoyote wa bodi ya Simba lakini pia hauna saini ya shahidi.
Pia,amesema katika kila nakala imesainiwa na Morrison pekee bila ya upande wa pili hatua ambayo inaoonyesha watani wao hao hawakuridhia mkataba huo.
“Una mapungufu makubwa katika sehemu mbili…hakuwa na shahidi lakini amesaini kwenye upande wake, CEO wa Simba hajasaini. Simba SC haijaridhia mkataba wa Morrison kwa sababu hakuna sehemu yoyote ambapo klabu ya Simba imesaini mkataba wa Morrison.
"FIFA inamtambua Morrison ni mchezaji wa Yanga. TMS ya FIFA inamtambua Morrison mchezaji wa Yanga. Mkabata wa Simba na Morrison una dosari, upande wa mchezaji umesainiwa bila shahidi,” amesema Makamu Mwenyekiti Yanga, Fredrick Mwakalebela.
Usajili wa Morrison kutoka Yanga kuibukia Simba umekuwa na sarakasi nyingi tangu awali ambapo mwanzo kulikuwa na mvutano mkubwa kati ya mchezaji na mabosi wake wa Yanga.
Yanga walikuwa wakieleza kuwa mchezaji huyo ana dili la miaka miwili huku mchezaji akieleza kuwa ana mkataba wa miezi sita na umemalizika.
Utata huo ulifanya suala hilo kutinga makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambapo kesi yake iliskilizwa kwa muda wa siku tatu mfululizo na hukumu ilitolewa kwamba Morrison ni mchezaji huru kwa kuwa mkataba wake na Yanga ulikuwa na mapungufu.
Kwa sasa limeibuka tena sakata hili ambalo nalo linaeleza kuwa bado Morrison mkataba wake ndani ya Simba una mapungufu muda ambao dirisha la usajili limefungwa na mchezaji huyo akiwa ameshacheza mechi ndani ya Simba.
Roho mbaya imemjaa
ReplyDeleteduh jamaa kiboko
ReplyDeleteKwa hiyo TFF wamemtambua vipi na kumruhusukuchezea simba au ndio mwasho wa tarehe 18/10. Unataka kuwapoteza simba wenzako wana bodi ya usajili sio kama nyinyi
ReplyDeleteHao yanga wamechanganyikiwa tu na Morrison,wanawaza tar 18 itakuwaje, mkataba wa Simba na Morrison unawahusu nn wao yanga,mchezaji ndo huwa analalamika juu ya mkataba wake,Simba inawachezaji 30 hakuna mchezaji alielalamika kuhusu mkataba wake,,,Sasa hao yanga wanahangaika kuchunguza mikataba ya wachezaji wa timu nyingne inawahusu nn,unahangaika na mke wa mtu kujua Kama mme wake amesain cheti Cha ndoa au hajasain,ili iweje
ReplyDeleteInawezekana ndio nyaraka alizowapelekea senzo
DeleteHizo nyaraka zipo CAS na siyo Senzo. Kwani Senzo ndio anamiliki CAS? Endeleeni na ushabiki ila hili jambo ni gumu sana kwa Simba na wakizubaa watanyang'anywa points zote katika mechi Morison alizocheza
DeleteNdio mnavyodanganywa mtazidi kupata stress
DeleteViongozi wa Simba ebu fukueni ile sakata la Mwakalebela kuongea na chama ilihali akiwa na mkataba...anawashwa huyu anahitaji kukunwa vizuri tarehe 18/10
DeleteHivi Kwa akili zenu unafikiri Simba wanakurupuka hawana wanasheria?
DeleteUtopolo Senzo anawapoteza msije juta, toeni matokeo ya CAS acheni blaablaa. Mmeshaliwa na GSM mmeliwa tu.
ReplyDeleteHii sasa inaitwa danganya toto. Kama mkataba haujasainiwa na simba huyo morisson angekubali vipi kucheza simba bila mkataba ili hali anajua kilichomtokea yanga? Mikataba yote ya wachezaji wa yanga anasaini gsm, kwani ndio kiongozi wa yanga?
ReplyDeleteWaambie hao! Waambie.
DeleteHaiingii akilini kabisa. TFF ingemruhusuje mchezaji kuchezea Simba kama mkataba ulikuwa na mapungufu? Morrison angepataje kibali cha kazi kutoka wizara husika bila mkataba uliokamilika? TFF ndiyo iliyoondoa jina la Morrison kwenye orodha iiyopelekwa TFFna Yanga na badala yake likabakia Simba. Hii ni baada ya kujirishisha document muhimu zote za mchezaji zilishakamilka kikiwepo kibali cha kazi
DeleteYanga mnataka point Simba anyang'anywe ili mchukue ubingwa kwa makando kando kweli nyie makando kando fc chezeni mpira mnazalilisha wachezaji wenu kuonekana si kitu mbele ya Morrison basi wapeni ubingwa yanga tff na ligi iishe basi
ReplyDeleteTrue, uwanjani wanechemka wanataka ushindi wamezani.
DeleteMagori kawajibu vizuri mkataba unawahusu Simba, Morison, FIFA na tff wao yanga huo mkataba wameupataje
DeleteMwakalabela akimaliza atuambie tonombe na yule nyoshi wamewasajili au wapo kwa mkopo. Yanga wamekuwa wanasheria
ReplyDelete