October 13, 2018


Aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal Thierry Henry ameteuliwa kuwakocha mkuu wa Monaco mpaka Juni 2021.

raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 41, ambaye amewahi kuwa naibu meneja wa timu ya tiafa ya Ubelgiji, alianza taaluma ya kucheza soka ya kulipwa katika klabu hiyo ya Monaco na aliisaidia kushinda taji la Ligue 1 mnamo 1997.

Klabu hiyo ipo katika nafasi ya tatu kutoka chini katika Ligue 1 na ilimtimuwa meneja aliyekuwepo Leonardo Jardim siku ya Alhamisi.

"Inaonekana kwamba ni hatma yangu kuwa nitaanza kazi kama meneja wa timu ya soka hapa ," amesema Henry, ambaye ameweka rekodi ya ufungaji magoli katika timu ya Arsenal

Mchezaji huyo wa zamani wa timu za Juventus, Barcelona na ya New York Red Bulls alihusishwa kuelekea Aston Villa katika wiki za hivi karibuni na anasema alipata maombi ya kufurahisha na kuvutia katika miezi kadhaa hivi nyuma.

"Daima Monaco itakuwa moyoni mwangu," aliongeza. "Nimefurahi sana kupewa fursa hii lakini sasa kazi ngumu ni lazima ianze."


Monaco imeshinda mara moja katima msimu kwenye mashindano yote. Katika Ligue 1 wanapointi 6 kutoka mechi 9 huku wakishindwa maa tano na wameshindwa mechi zote katika ligi ya mabingwa.

Mechi ya kwanza atakayoisimamia Henry itakuwa dhidi ya Strasbourg ikatika ligi ifikapo Oktoba 20, kabla ya mtanange katika ligi ya mabingwa na Club Brugge siku nne baadaye.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic