August 22, 2021



IKIWA ni kuelekea katika wiki ya Mwananchi ambapo kilele chake kinatarajiwa kiwa Agosti 29, Uwanja wa Mkapa tayari harakati zimeanza kwa jamii.


Jana Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Klabu ya Yanga, Saady Khimji kwa kushirikiana na viongozi wenzake wa Makao Makuu lakini pia WanaYanga Zanzibar na Serikali walikabidhi magodoro 30 Hospitali ya Mwemberadu Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.


Mgeni Rasmi wa Shughuli hiyo alikuwa Waziri wa Ardhi na Makazi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Riziki Juma Pembe.


Ni Khimji aliongoza msafara wa uongozi kutoka makao makuu akiwa ni mwakilishi wa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dr. Mshindo Msolla ambaye alipata dharura iliyomfanya ashindwe kufika katika uzinduzi huo Zanzibar.


Mara baada ya kukabidhi Magodoro hayo Msafara wa Uongozi wa Yanga ulielekea Mkoa wa Kusini Unguja eneo la Ukongoroni kufungua tawi na kuweka jiwe la msingi katika jengo la Yanga lililopo hapo.


Leo shughuli rasmi za uzinduzi zitaanza saa moja asubuhi kwa maandamano kuelekea Kisiwandui na baadae kwenye Mkutano wa Wanachama wote utakaofanyika Ukumbi wa NSSF uliopo eneo la Kariakoo Zanzibar.

8 COMMENTS:

  1. Hayo magodoro kwa hospitali ni stahiki kweli? Mbona kama ya nyumbani nyumbani

    ReplyDelete
  2. Kusudio ni kutafuta kuonewa huruma kwa kukosa ubingwa kwa miaka mine mfululizo ili safari hii waonje kitu lakini kwa mtazamo Mnyama ataendelea kunguruma na waendelea kujidanganya

    ReplyDelete
    Replies
    1. Itakuwa kwenye ligi ya zanzibar sababu tukio lipo zanzibar

      Delete
  3. Wengi wetu huku ni wapenzi wa rangi nyekundu

    ReplyDelete
  4. Kweli nyie akili zenu zinawatosha wenyewe muko tofauti na binadamu wenzenu godoro hazifai sawa je wewe umepeleka nn hosptal hata damu kuchangia hamuwezi badilikeni ushabiki wa kizamani huo

    ReplyDelete
  5. Hoja za Watopolo hafifu wala hazina mana wala haziingii akilini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ww Kwa mwez huu umepeleka nn hosptal kamahuruma kwa wagonjwa

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic