February 7, 2016


Hatimaye kocha Jose Mourinho amevunja ukimya na kuzungumza kwa mara ya kwanza tokea atimuliwe Chelsea FC.

Mourinho ambaye aliipa ubingwa timu hiyo msimu uliopita, sasa anahusishwa na kujiunga na Manchester United huku Louis van Gaal akisubiri kutimuliwa.

Akiwa katika harakati zake za kuitangaza gari aina ya Jaguar, Mourinho ,53, amesema hivi karibuni atarejea katika soka.


“Kila mara ninajifunza, hata katika sehemu ambayo ninaamini mimi ni mtaalamu, bado ninaendelea kujifunza mambo mapya.

“Najua watu wengi wanaamini mimi si msikivu au mnyenyekevu, wanakosea. Mimi ni binadamu wa kawaida kabisa ambaye si sahihi na ninapenda kujifunza,” alisema Mourinho aria wa Ureno aliyewahi kuzifundisha FC Porto, Inter Milan na Real Madrid.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic