February 7, 2016

BAADHI YA WACHEZAJI WA GENK WAKIWA NDANI YA BASI LA KLABU HIYO...

  
Mtanzania Mbwana Samatta ameishaanza kuichezea KRC Genk ya Ubelgiji baada ya jana kuingia katika mechi ya ligi na kucheza kwa dakika 17 wakati timu hiyo ilipoivaa Mouscron na kushinda kwa bao 1-0.

Akiwa Ubelgiji, mara nyingi atakuwa akitumia usafiri wa kijamii, yaani treni. Lakini kwa shughuli za timu, Samatta atakuwa akitumia basi la wachezaji.
Samatta anaonyesha ni mtu wa malengo kweli baada ya kuacha magari yake zaidi ya matatu, na kwenda kuanza kutafuta maisha upya Genk.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa TP Mazembe, ameamua kuachana na kila kitu ukiwemo umaarufu wake mkubwa nchini DR Congo na kwenda kuanza upya nchini Ubelgiji kwa kuwa anataka kutimiza ndoto yake.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic