February 10, 2016

MISHETTTO
Mtanzania Charles Mishetto ameondoka Ujerumani na kwenda kufanya majaribio katika klabu moja nchini Jamhuri ya Czech.

Taarifa za uhakika zimeeleza, Mishetto aliyekuwa anaichezea Rabestein FC inayoshiriki Ligi Daraja la Nne nchini Ujerumani sasa yuko Jamhuri ya Czech.

“Kweli Mishetto yuko Czech anafanya majaribio, ninajua ni timu ya daraja la pili, ila sijajua ni timu gani. Iwapo atafanikiwa au kutofanikiwa nitakutaarifu,” kilieleza chanzo kutoka Ujerumani.

Rabestein FC inashiriki Ligi Daraja la Nne nchini Ujerumani na Mishetto alikuwa mmoja wa wachezaji tegemeo.


Mishetto amewahi kukipiga Stand United ya mjini Shinyanga kabla ya kuanza kupambana kutafuta maisha ya soka barani Ulaya.

Juhudi za kumpata Mishetto mwenyewe aweze kufafanya hilo bado zinaendelea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic