Wachezaji wa timu ya mchezo wa raga walilazimika kuacha mechi na kupanda jukwaani kwenda kuwaokoa wake na watoto zao waliokuwa jukwaani.
Wake na watoto za wachezaji wa timu ya Salford Red Devils walikuwa wanashambuliwa na mashabiki baada ya timu hiyo kupoteza mchezo
Ilikuwa ni mechi ya Kombe la First Utility Super League kati ya Salford Red Devils dhidi ya Huddersfield Giants kwenye Uwanja wa John Smith katika eneo la West Yorkshire nchini England.
Wachezaji hap walitembeza timbwili la uhakika hadi walinzi wa uwanja walipoingilia na kuzima vurugu hizo.
0 COMMENTS:
Post a Comment