March 29, 2016


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema kutakuwa na kipindi cha mazoezi magumu ili kukiimarisha kikosi chake zaidi.

Pluijm raia wa Uholanzi amesema wanalazimika kufanya mazoezi hayo ili kujiweka sawa zaidi kwa stamina na kasi.


“Mechi zinazokuja ni nyingi, nafikiri tungepata muda zaidi wa kujiandaa na Al Ahly. Lakini bado tunahitaji stamina zaidi,” alisema.

“Hofu ni suala la uchovu, hakika ni mechi nyingi sana kwa kipindi kifupi ambalo si jambo zuri kwetu,” alisema.


Yanga inatarajia kufanya mazoezi leo jioni jijini Dar ikiwa ni sehemu ya kujiendeleza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV