May 9, 2016


Baada ya hivi karibuni Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuipa taarifa Klabu ya Simba kutakiwa kumlipa aliyekuwa beki wake, Mkenya Donald Mosoti, uongozi wa timu hiyo umetamka kuwa unajipanga kuhakikisha unamalizana na beki huyo kwa kumpa chake.

Fifa ilitoa barua kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya kuwataka Simba kumlipa beki huyo mrefu wa jumla ya Sh 70.2 ikiwa ni malipo ya mchezaji huyo pamoja na faini ya kuzembea kumlipa na endapo watashindwa kumalizana na beki huyo ndani ya siku 30, watashushwa daraja. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema: “Tayari tunafahamu kuwa tunatakiwa kumlipa aliyekuwa beki wetu, Donald Mosoti fedha zake baada ya kuachana na sisi yakiwa ni maagizo kutoka Fifa na hatuwezi kulipinga suala hilo kutoka kwa chombo hicho kikubwa.

“Unajua Mosoti wakati tunaachana naye tulichofanya ni kulikata jina lake katika mashindano ya ligi kuu lakini tukaliacha katika mashindano mengine yote ambayo tulikuwa tunashiriki lakini yeye akaona kuwa anataka kucheza zaidi, hivyo ndiyo tukaachana naye.

“Lakini kwa sasa tunajipanga kuona tunamalizana naye na kumpa fedha zote anazotudai kwani hiyo adhabu ya kushushwa daraja siyo kitu kidogo na endapo suala hilo litakuja kutokea, wanachama wanaweza wasituelewe,” alisema Hans Poppe.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic