May 9, 2016


Bao la dakika za mwisho lililofungwa na straika wa Yanga, Matheo Anthony, juzi Jumamosi, lilimtoa machozi Kocha Mkuu wa Sagrada Esperanca, Zoram Manojlovec, raia wa Serbia na kutamka wazi kuwa safari yao kwenye michuano ya kimataifa ndiyo imeishia hapo.

Matheo alifunga bao hilo kwa shuti kali akiwa nje ya eneo la hatari la Esperanca katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar na kuifanya Yanga kuondoka uwanjani na mabao 2-0 huku bao la kwanza likifungwa na Simon Msuva dakika ya 72.

Manojlovec amesema, awali walijua kwamba mchezo utamaliza wakiwa wamefungwa bao 1-0, lakini walishangaa ikiwa imebaki dakika moja kabla ya mpira kumalizika wakaruhusu bao hilo.

“Matokeo yangebaki 1-0 yangekuwa nafuu kwetu, lakini haya ya 2-0 yametufanya tuwe kwenye wakati mgumu, lakini naamini kwenye soka lolote linawezekana japo haitakuwa rahisi kuwatoa Yanga.


“Lile bao la mwisho ndiyo liliwamaliza kabisa wachezaji wangu pamoja na benchi zima la ufundi kwani tuliamini kwamba mpira ushamalizika, cha kushangaza dakika ya mwisho tunaruhusu bao, kwa kweli limetumaliza kabisa,” alisema Manojlovec.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV