July 9, 2016


Uongozi wa Klabu ya Royal Eagles inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Afrika Kusini, umemnyang’anya hati ya kusafiri ‘paspoti’ winga wao, Uhuru Selemani.

Hatua hiyo imekuja siku chache tangu arejee nchini humo akitokea Tanzania kwa mapumziko ambapo adhabu hiyo ni mwendelezo wa kosa la kucheza mechi za mchangani maarufu kwa jina la ndondo wakati akiwa mapumziko hapa nchini.

Uhuru amesema kuwa, aliandika barua ya kuomba msamaha kwa uongozi wa timu hiyo, lakini hadi hivi sasa hajajibiwa huku akiendelea kujifua kivyake ufukweni.

“Nilipanga kurejea Dar, wiki hii kwa ajili ya kukaa na familia baada ya kusimamishwa na uongozi wa timu yangu, lakini imeshindikana baada ya kuninyang’anya paspoti yangu.

“Tofauti na kusimamishwa kwenye timu, upo uwezekano wa kupigwa faini na kutolipwa mshahara wangu wa miezi miwili, wameninyang’anya kwa kuwa wanahofu naweza nikahama timu,” alisema Uhuru.


Imekuwa ni kawaida ya wachezaji wengi nchini kucheza mechi za ndondo hasa wanapokuwa katika mapumziko ya ligi mbalimbali licha ya baadhi yao kukatazwa na timu zao.

SOURCE: CHAMPIONI 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic