July 9, 2016


Unaweza ukasema hadi kieleweke.Kwani sasa Simba imethibitisha ujio wa mshambuliaji wao mpya waliyekuwa wakimsaka kwa muda mrefu, Laudit Mavugo atakuja nchini keshokutwa Jumatatu.

Simba msimu uliopita ilikwama kumsajili Mavugo kwani haikuweza kukubaliana bei na timu yake ya Vital’O ya Burundi licha ya kutanguliziwa fedha, lakini sasa mambo yanaonekana kuwa ‘fresh’.

Kwa siri sana, mmoja wa mabosi wa Kamati ya Usajili ya Simba, amesema kuwa, mipango ya kumleta Mavugo bado ipo palepale na anatarajiwa kutua nchini Jumatatu ijayo tayari kwa kujiunga na timu yao.

“Vital’O wameamua kumjumuhisha Mavugo katika kikosi huku wakijua mchezaji huyo amemaliza mkataba na kudai kuwa straika huyo ni mali ya Simba kwa sasa.


“Mavugo tayari aliingia mkataba kwa dau la Sh milioni 36 tangu msimu uliopita, tunatarajia atakuja Jumatatu, ataingia kambini na timu kati ya Zanzibar au Morogoro,” alisema bosi huyo.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV