July 15, 2016


Kocha Mkuu wa Mwadui FC ya mkoani Shinyanga, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amefunguka kuwawachezaji wa kimataifa wanaokuja kucheza soka nchini, wengi wao ni waganga njaa kutokana na kutokuwa na uwezo wa juu kisoka.

Julio ambaye msimu uliopita alimaliza ligi timu yake ikiwa katika nafasi ya sita kwenye Ligi Kuu Bara, ameeleza kuwa, hana pupa na usajili kwa kuwa hahofii usajili wa timu kubwa na badala yake anafanya mambo kwa mahesabu ili kuweza kupata wachezaji wenye viwango.

Julio ameeleza kuwa, hana mpango wa kuleta wachezaji wa kigeni katika kikosi chake kutokana na kutambua kuwa wengi wao wapo kimaslahi zaidi na wanakuja kuganga njaa Bongo huku vipaji vyao vikiwa ni vya kawaida.

“Mimi nina mpango wa kupunguza kikosi msimu huu ambapo msimu uliopita nilisajili wachezaji 33 lakini kwa sasa nitasajili wachezaji 23 kati ya hao, makipa watatu na wachezaji wa ndani 20.

“Sina haja ya kusajili maprofesheno kwani asilimia kubwa wapo hapa kwa ajili ya kuganga njaa tu, hawana kiwango chochote. Wachezaji ambao ni maprofesheno ambao wapo vizuri wanaocheza ligi kuu ni Ngoma (Donald), Tchetche (Kipre) na Wawa (Pascal) waliobakia wote hakuna kitu, wanaganga njaa tu,” alisema Julio.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic