July 14, 2016


Mbwana Samatta amefunga bao moja na kuiwezesha KRC Genk ya Ubelgiji kushinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Buducnost Podgorica katika mechi ya kuwania kucheza Europa Cup. Genk ilikuwa nyumbani.

Samatta alifunga bao hilo katika dakika ya 79, baada ya Kebano kuwa amefunga la kwanza katika dakika ya 17 kwa mkwaju wa penalti.

Samatta aliunganisha vizuri krosi ya Kebano na kufunga bao hilo la pili muhimu dhidi ya timu hiyo kutoka Montenegro. Ushindi ni muhimu kwa kuwa ni sawa na kikosi cha Genk kinaongoza kwa mabao 2-0.

VIKOSI:
KRC Genk : Bizot, Castagne, Dewaest, Kumordzi, Uronen, Ndidi, Buyens (73 'Heynen) Kebano (76' Karelis), Bailey, Buffalo and Samatta (87 'Trossard).


Buducnost Podgorica : Dragojevic, Vusurovic (84 'Camaj), Mitrovic, Vukcevic, Radunović, Pejakovic (74' Seratlic) Raickovic (59 'Janketić), Hoko, Đalović, Mirkovic, Raspopovic

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV