November 3, 2016


Ushindi wa mabao 2-1 walioupata Mbeya City dhidi ya Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, jana unakuwa mtihani mwingine kwa Yanga.

Yanga wanaingia kwenye mtihani huo kutokana na mechi inayofuatia dhidi ya Prisons ambao wanakutana nao Jumamosi.

Prisons ambao wanashindana kwa juhudi zote na Mbeya City, hawatakubali kuona wao wanaishindwa Yanga kwa mambo mawili.

Kwanza ni kwa ajili ushindani wao mkali dhidi ya Mbeya City ambao wamewaonyesha wamewaweza Yanga, vipi wao washindwe?

Pili wanachuana na Mbeya City kwa pointi, Prisons sasa wana 16 na wasingependa kuzidiwa zaidi kwa kuwa sasa tayari Mbeya City wana 19.

Kufanikisha yote haya, lazima Prisons washinde ili kuwakimbiza wapinzani wao Mbeya City, pia kuwaonyesha hakuna wanachoshindwa pia.

.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic