November 3, 2016


Baada ya kuitwanga Stand United iliyokuwa haijawahi kufungwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga msimu huu, Simba imenogewa na pointi.

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema wanataka kumalizia mechi mbili zilizobaki za mzunguko wa kwanza kwa ushindi pia.

“Kwanza nikuambie ligi bado ni ngumu, lakini tunapenda kushinda mechi mbili za African Lyon na Prisons. Halafu tutaanza kujipanga kwa mzunguko wa pili,” alisema.

Simba ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 35 kileleni, tofauti ya pointi nane na Yanga wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 27.

MECHI ZA SIMBA ZA MZUNGUKO WA KWANZA:
NOV 6     Vs African Lyon
NOV 9      Vs Prisons 0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV