December 11, 2016





Wanachama wa Simba wamekutana leo na kwa pamoja kupitisha kipengere ambacho kitaruhusu mabadiliko yatakayowezesha suala la kukodisha au uwekezaji.


Mkutano huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polis jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wanachama 642 hai.

Zoezi hilo lilichukua zaidi saa nne na kila kitu kikienda vizuri huku Mwanasheria, Evodius Mtawala ambaye aliwahi kuwa katibu mkuu wa Simba akipewa nafasi ya kutoa ufafanuzi wa vipengele vya katiba, kisheria.



Wanachama takribani 19, wao walisema hapana katika baadhi ya marekebisho ya vipengele kadhaa wakati wakitakiwa kusema ndiyo hapana.

Hata hivyo, idadi kubwa ilionyesha kuwa na hamu ya kufanyika kwa marekebisho ili wawekezaji wapate nafasi ya kuingia.

Kinachobakia ni kuwasilisha uamuzi huo wa mabadiliko kwa Baraza la Michezo la Taifa (Basata).

Rais wa Simba, Evans Aveva na jopo la uongozi wa klabu hiyo, walihudhuria mkutano huo ambao ulitawaliwa na amani.



Katika mkutano huo, ajenda saba zilikuwa hizi:

1. Uhakiki wa wanachama waliohudhuria mkutano.

2. Kufungua mkutano.

3. Hotuba ya Rais

4. Kusoma na kujadili mapendekezo ya mabadiliko ya katiba

5. Kupiga kura mapendekezo ya mabadiliko ya katiba

6. Majumuisho ya mapendekezo ya mabadiliko ya atiba


7. Kufunga Mkutano

Simba wamekubaliana kufanya mabadiliko
642

19

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic