December 11, 2016



Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa nafasi kwa wafamilia wa soka kupendekeza majina ya timu za Taifa za vijana wenye umri wa chini ya miaka 23 za wanawake na wanaume.

Timu hizo za Taifa ya Wanawake U23 na Timu ya Taifa ya Wanaume U23, zitaingia kwenye program ya kuandaliwa kuwania nafasi ya kucheza fainali za michuano ya Olimpiki zitazayofanyika jijini Tokyo, Japan; mwaka 2020.

Wadau wa mpira wa miguu wanaombwa kupendekeza majina hayo kupitia anwani za tanfootball@tff.or.tz, mjselestine@yahoo.co.ukau Namba za simu +255 678 297727, +255 624 121812, +255-22-2182032 au nukunishi (faksi) +255-22-2182031.

Tayari Tanzania ina majina ya timu za Taifa ya wanaume wakubwa (Senior National Team) ambayo ni Taifa Stars, Timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania ‘Twiga Stars’ na Timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Queens’.
.

Pia zimo timu ya Taifa ya Vijana ya wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’; Timu ya Taifa ya wanawake wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘The Tanzanite Queens’ na timu ya Taifa ya Vijana ya wenye umri wa chini ya mika 17 ‘Serengeti Boys’

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic