December 23, 2016




Yanga imepangwa kuanza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuwavaa Ngaya de Mbe ya Comoros.

Kocha wake, George Lwandamina amesema haitakuwa kazi rahisi na Yanga haitafanya mzaha hata kidogo.

"Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni mikubwa na migumu, inakutanisha mabingwa wa nchi za Afrika. Hauwezi kuidharau timu yoyote," alisema.

Yanga ikifanikiwa kuwaondoa Wacomoro, itakutana na kati ya Zanaco ya Zambia au APR ya Rwanda ambazo ni timu ngumu.

Chini ya Lwandamina, Yanga imekuwa ikiendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic