Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) na Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza (MZFA), wametoa muda
kwa Klabu ya Toto Africans kufanya uchaguzi mwishoni mwa mwezi huu na kama
wasipofanya hivyo, timu hiyo itashushwa daraja.
Mwenyekiti wa MZFA, Jackson Songora amesema kuwa klabu
hiyo imepewa muda kufikia mwishoni mwa mwezi huu lazima iwe imeshafanya
uchaguzi, bila hivyo timu hiyo inaweza kushushwa daraja.
Songora
alisema klabu hiyo imekuwa na mivutano ambayo haina msingi na kusababisha pia
kusuasua hata kwenye mechi zake za Ligi Daraja la Kwanza.
“Toto
wanatakiwa kufanya uchaguzi kabla ya mwezi huu kumalizika, hatutaki kuona
migogoro ya mara kwa mara ambayo inasababisha timu kufanya vibaya,” alisema
Songora.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment