Azam FC imeendeleza vipigo baada ya kushinda mechi yake ya sita
huku ikiwa na sare moja.
Ikiwa ugenini, Azam FC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
wenyeji wake Ndanda FC katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda
mjini Mtwara.
Azam FC imepata ushindi kwa bao pekee lililofungwa na beki wake wa kulia, Shomari Kapombe.
Pamoja na mechi kuwa nzuri, hali ya uwanja ilionekana kuwapa
wakati mgumu wachezaji wa Azam FC.
Kutokana na ushindi huo, Azam FC imefikisha pointi 19 sawa na
Yanga ambayo iko kileleni na Azam Fc inabaki katika nafasi ya pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment