April 2, 2013



 
Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic amekuwa mwiba mkali kwa timu yake ya zamani ya Barcelona baada ya kufunga bao la kwanza na kutoa pande lililozaa la pili katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya timu hiyo.


PGS iliyokuwa nyumbani imelazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya Barcelona ambayo ilitangulia kupata bao lake kupitia kwa Lionel Messi lakini Ibra Kadabra akasawazisha.

Baadaye Barcelona ikapata bao la pili kwa mkwaju wa penalti uliowekwa kimiani na nahodha Xavi la Ibra akatoa pasi kwa Metuidi ambaye alipiga shuti la chinichini lililojaa wavuni.


Kiungo mpya wa PSG, David Beckham alichemsha na kutolewa na majibu sahihi nani amesonga hadi nusu fainali yatapatikana wiki ijayo baadaye katika mechi ya marudiano.



Upande Bayern Munich wakiwa nyumbani, waliwachosha wakali wa Italia Juventus kwa kuwapiga kwa mabao 2-0.

Mabao ya Bayern ambao wanaonekana kushika kasi kama gari lililokosa breki yalifungwa na Alaba na Muller, hivyo kujiweka katika mazingira mazuri katika mechi ya marudiano jijini Turin, Italia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic