December 13, 2017



Straika mpya wa Yanga, Yohana Nkomola, ameungana rasmi na wachezaji wa Yanga kwenye mazoezi yao baada ya kutoka katika majukumu ya timu ya taifa Taifa Stars ikiwa ni siku moja tu baada ya kutua nchini akitokea kwenye kikosi hicho. 

Straika huyo ambaye tangu asajiliwe na Yanga hakuwahi kufanya mazoezi na kikosi hicho kutokana na kuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa, leo kwa mara ya kwanza amefanya mazoezi ya pamoja na wenzake huku akikutana uso kwa uso na washambuliaji wenzake kama Amissi Tambwe pamoja na Kiungo Papy Tshishimbi.


Yanga imeendelea na mazoezi ya uwanjani leo, yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar, kwa ajili ya maandalizi ya michuano ile ya FA pamoja na Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuendelea hivi karibuni.

1 COMMENTS:

  1. KUNA HIKI KITU...:
    Sijajua mkataba unasemaje wa Sportpesa au Vodacom kuhusu matumizi ya vifaa vitokanavyo na wadhamini. Wenzetu kule walipoendelea wanathamini sana uwepo wa Mdhamini wao. sijajua kama tayari Yanga imeanza kuntumia vifaa vya CAF badala ya Vodacom au Sportpesa. Turudi kwa kuliangalia hilo. Tufanye vitu kisomi. Hata Sportpesa wenyewe sijui kama wanalifuatilia hilo...na kama hawajatoa BIBs kwa ajili ya mazoezi watakuwa wamekosea sana kwani Nembo yao itabidi ifunikwe na Taswira ya CAF kifuani.

    Hili pia nimeliona kwenye Benchi la SIMBA SC...utakuta kocha kavaa track ya Sportpesa alafu amevaa Kofia ya Adidas au yoyote ilimradi ni nyekundu. Hili ni kosa katika mkataba ni bora asivae kabisa kama Babu Hans. Sportpesa inabidi waangallie hili tatizo halijaanza leo...najua tangu ipo vodacom kifuani kwa simba lakini kocha alikuwa anavaa kofia nyekundu ya Adidas au yoyote ile.

    NAOMBA:
    Naomba tuzingatie mikataba tunayoingia na wadhamini katika hili ili tufanye kazi kwa uweredi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic