January 19, 2018



Ule msafara wa kikosi cha Simba unatarajiwa kupanda ndege leo Ijumaa kuelekea mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar katika Ligi Kuu Bara utakaochezwa wikiendi hii.

Safari hiyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya timu hiyo kuifunga Singida United mabao 4-0, jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Simba itatua mjini Bukoba ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 2-1 ilichokipata msimu uliopita.

Mechi hiyo ilizuia mtafaruku mkubwa na Simba walidai ndiyo iliyowakosesha ubingwa.


Hii ilitokana na madai yao kwamba Kagera walimchezesha beki wao Fakhi Mohammed akiwa na kadi tatu za njano. Mwanzo walishinda lakini baadaye pointi tatu zikawatoka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic