February 19, 2018


Kikosi cha mabingwa wa Tanzania, Yanga watafanya mazoezi yao ya kwanza nchini Shelisheli, leo.

Kikosi hicho chini ya Lwandamina kitafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Unity ambao utachezewa mechi hiyo.

Yanga inakwenda mazoezini saa tatu asubuhi kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kuwavaa St Louis katika mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0. Jambo linaloilazimu kuhakikisha inashinda tena au kupata sare katika mechi hiyo ya ugenini.

Yanga ilitua nchini humo jana ikipitia Nairobi na Meneja wa kikosi hicho, Hafidh Saleh amesema wako tayari kwa kazi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic