Baadhi
ya wachezaji wa Azam FC huenda wakaingia katika mtego wa adhabu kutoka kwa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) hasa kama kamisaa wa mchezo wao dhidi ya
Yanga ataandika kuhusiana na ilivyokuwa.
Mara
baada ya mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ambao walilala kwa bao 1-0,
wachezaji wa Azam FM walimvamia mwamuzi wa mchezo huo wakimlaumu kwamba muda wa
ziada haukuonyeshwa.
Baadhi
ya wachezaji wa Azam FC walidiriki kumsukuma mwamuzi huyo ambaye baada ya nusu
dakika alikuwa katika wakati mgumu hadi askari polisi walipolazimika kuingia
uwanjani kumuokoa.
Hata
pamoja na askari hao kuingia uwanjani, bado wachezaji wa Azam FC waliendelea
kupandisha jazba wakibishana na baadhi ya askari hao.
Mwisho,
askari hao walitoka na mwamuzi huyo akiwa chini ya ulinzi mkali unaokaribia ule
anaopewa rais wan chi hasa anapokuwa katika msongamano wa watu wengi.
Lolote
linaweza kutokea lakini ripoti ya kamisaa ndiyo inaweza kuwa jibu la mwisho
kuhusiana na kilichotokea katika mechi hiyo iliyohudhuriwa na watu wengi zaidi
kuliko nyingine tokea mzunguko wa pili ulivyoanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment