September 29, 2019


Beki wa Real Madrid Dan Carvajal ametoa jumla ya assisti tatu kwenye mechi za La Liga huku timu yake ikiwa imefunga jumla ya mabao 12 kwenye mechi saba ambazo wamecheza mpaka sasa.

Madrid kwa sasa ni vinara wa La Liga baada ya kucheza jumla ya michezo Saba na kujikusanyia pointi 15 huku Barcelona ikiwa nafasi ya nne na ina pointi 13.

Jana ililazimisha sare ya bila kufungana na watani wao wa jadi Atletico Madrid ambao wanashika nafasi ya tatu wakiwa wamejikusanyia pointi 14.

Mchezo wao unaofuata itakuwa ni Jumanne utakuwa ni wa UEFA na ule wa La Liga utakuwa ni Octoba 5 na itamenyana na Granada.

Granada ipo nafasi ya pili ikiwa imecheza jumla ya michezo Saba na imejikusanyia pointi 14 baada ya kushinda mechi nne, sare mbili na kupoteza mchezo mmoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic