February 18, 2013



BAADA ya kiungo nyota wa zamani wa England, Paul Ince kupewa kazi ya kuifundisha Blackpool, kitu cha kwanza kilichozua gumzo si kazi yake hiyo badala yake ni mwanaye.
Ince aliyewahi kung’ara akiwa na Man United na baadaye Inter Milan na Liverpool, ameingia mkataba wa mwaka mmoja kuinoa Blackpool baada ya kocha wa zamani kutupiwa virago.
Kinachowavutia wengi zaidi, Ince aliyekuwa mkorofi wakati wa enzi zake, atakuwa bosi wa mwanaye Tom Ince ambaye ni mmoja wa wachezaji tegemeo wa Blackpool.
Hata hivyo, Ince tayari ameonyesha kutotaka ishu ya mwanawe iwe gumzo kubwa zaidi, badala yake watu waangalie Blackpool inasonga vipi mbele.
Wakati Fulani, Ince aliwahi kumshambulia kocha wake wa zamani, Alex Ferguson kwa madai alikuwa akifanya kazi na mwanaye na kutaka kuifanya timu hiyo kama familia.
Ince ameona mwelekeo wa wadau wengi ni huko, naye amekuwa mwepesi kukumbushia huku akisisitiza, aachwe afanye kazi yake.
 Kuonyesha amepania kuifanya kazi yake vizuri, Ince ameutaka uongozi wa Blackpool kumbakisha kocha msaidizi, Steve Thompson ili aendelee naye.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic