February 18, 2013


Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete amesema iwapo wataifunga Azam FC katika mechi yao Jumamosi, hakuna atakayewazuia kuchukua ubingwa.
Akizungumza na Salehjembe, Tegete alisema ana uhakika mechi hiyo ndiyo majibu ya njia yao ya kutwaa ubingwa.
"Kama tukiwafunga Azam mimi nina uhakika Yanga itakuwa bingwa, lakini kama hatutashinda, bado tutakuwa na nafasi ya kuendelea kupambana.
"Kikosi chetu kina uwezo mkubwa lakini soka mambo mengi yanatokea hivyo hauwezi kujua. Lakini uhakika wa kushinda kwa maana ya ubora wa kikosi naweza kusema Yanga ina kikosi bora zaidi," alisema Tegete.
Yanga iko kileleni ikiwa na pointi 36 wakati Azam FC inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 33, hali inayofanya mchezo huo kuwa gumzo zaidi wiki hii. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic