July 8, 2018


Na George Mganga

Michuano ya Kombe la KAGAME katika hatua ya robo fainali inaendelea tena leo kwa mechi mbili kupigwa majira ya jioni.

Simba ambao ni mabingwa wa kihistoria katika mashindano hayo watakuwa Uwanja wa Taifa majira ya saa 1 usiku kucheza dhidi ya AS Ports kutoka Djibout.

Simba walifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kushinda mechi zake mbili dhidi ya Dakadaha FC ya Somalia na APR ya Rwanda huku ikienda sare ya 1-1 dhidi ya Singida United ambayo inashiriki mashindano haya kwa mara ya kwanza.

Wakati huo Simba ikitarajiwa kukipiga dhidi ya Ports, beki Pascal Wawa ambaye amehusishwa kuondoka japo uongozi ukikanusha taarifa hizo, anatarajiwa kuwa sehemu ya wachezaji watakaokuwepo kwenye kikosi hicho.

Wawa amefanya mazoezi na Simba jana Jumamosi kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam tayari kwa maandalizi ya kipute cha leo dhidi ya Wadjibout.

Kabla ya mechi hiyo, Gor Mahia FC kutoka Kenya wataanza kibarua cha hatua hiyo ya robo fainali kwa kucheza na Vipers SC kutoka Uganda kuanzia saa 10 kamili jioni. Mechi zote mbili zitachezwa katika Uwanja wa Taifa.

1 COMMENTS:

  1. WEWE MWANDISHI GANI UNAYELAZIMISHA HABARI ZA WAWA KUONDOKA WAKATI TAYARI KLABU YA SIMBA IMEKANUSHA? FIKIRIA UNAVYOMSONONESHA MCHEZAJI MWENYEWE KWA HABARI HIZO ZISIZO ZA KWELI HIVI UNADHANI UNAFANYA VIZURI?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic