April 5, 2013






Dalili za ndoto ya Yanga kuwa na uwanja wake wa kisasa zinakaribia kutimia baada ya Wachina kutoa ramani tatu ili uongozi wa Yanga uchagua.

Kampuni ya Wachina ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) imewapa yanga ramani ya viwanja vitatu, cha gharama zaidi kikiwa kinagharibu dola 50,000 (zaidi ya Sh bilioni 81) ili wachague wanachokihitaji.


Uongozi wa Yanga, ndiyo utafanya kazi ya kuchagua moja ya ramani kati ya hizo tatu ili kupata moja itakayotumika kwa ajili ya ujenzi.

Meneja Mkuu wa BCEG, David Zhang iliyojenga Uwanja wa Taifa, alikabidhi ramani hizo tatu kwa jopo la viongozi wa Yanga liliongozwa na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu hiyo, Francis  Kifukwe ambaye kiutaalamu ni injinia.


Uwanja huo wenye thamani ya dola milioni 50,000 utakuwa na uwezo wa kuchukua watu 50,000, mwingine una uwezo wa kubeba watu 40,000 na thamani yake ni dola milioni 40,000 (zaidi ya Sh bilioni 64.) na watatu utachukua watu 30,000 na thamani yake ni 30,000 (zaidi ya Sh bilioni 48).

Makabiadhiano hayo ya ramani, yalifanyika kwenye ofisi za Uwanja wa Taifa, Dar ambao umejengwa na kampuni hiyo.

Baada ya hapo, uongozi wa Yanga utafanya uchaguzi wa ramani moja itakayotumika na kuwataarifu Wachina hao ambao watakutana na uongozi huo na kuanza mjadala.

Hata hivyo inaonekana wajenzi wanahitaji eneo kubwa zaidi ya lile linalomilikiwa na Yanga katika eneo la Jangwani.

Tayari Yanga imepeleka ombi serikalini ili iongezewe kipande cha uwanja ili kuongeza walionao kwa ajili ya ujenzi.


Zhang alisema wametoa mapendekezo ya idadi ya watu kulingana na Yanga wanavyotaka watakaoingia uwanjani humo kwa gharama tofauti.

Uwanja unatarajiwa kuwa na Hotel ambayo inaweza kutumiwa kama kambi, chumba cha mikutano cha waandishi wa habari, ofisi mbalimbali pamoja na Supermarket.

Pia kutakuwa na vyumba vya kuvalia nguo wachezaji, chumba cha wafanyakazi, viti maalum kwa ajili ya matibabu, gym, bar pamoja na ukumbi mkubwa kwa ajili ya sherehe mbalimbali.

 “Bajeti ya Yanga ndiyo itakayoamua kukamilika kwa ujenzi huo mpya wa kisasa, wao wakiwa na bajeti uwanja huo utachukua hata mwaka mmoja.

 “Hekta 11 .5 za eneo zinahitajika katika ujenzi huo wa ujenzi na gharama zetu zinatofautina kulingana na idadi ya watu wanayotaka kuingia uwanjani humo ambazo zinapungua,” alisema Zhang.

 Kwa upande wa Kifukwe alisema wanatarajia kusaini mkataba huo wa ujenzi mwishoni mwa Mei, mwaka huu baada ya viongozi kukutana, kujadiliana na kukubaliana aina ipi ya uwanja wanayoutaka.

Kuhusu suala hilo, Kifukwe ambaye ni injinia wa mauala ya ujenzi na sasa ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ya Yanga, alisema:

 

“Tumeona ramani ya ujenzi ya uwanja jinsi utakavyojengwa, tunatarajiwa kukutana na viongozi hivi karibuni kwa ajili ya kutoa mapendekezo ya idadi ipi ya watu watakaoingia.

 “Uwanja huo unahitaji eneo kubwa kama hekta 11.5 kwa mujibu wa kampuni hiyo ya ujenzi, hivyo tunahitaji eneo zaidi ili uwanja ukamilike, tunasubiria majibu kutoka kwa serikali na manispaa ambao tumemaomba watuongezee eneo lingi.”

Yanga chini ya uongozi wa Yusuf Manji imekuwa ikihaha kutekeleza ahadi ya kuwa na uwanja wake wa kisasa ambao utakuwa ukitumika kwa ajili ya mechi mbalimbali.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic