Chelsea
imeendelea na mwendo mzuri katika michuano ya Europa baada ya kuichapa Rubin
Kazan kwa mabao 3-1.
Mshambuliaji
wake, Fernando Torres ‘Nando’ amerudi nyavuni mara mbili baada ya kufunga bao
katika dakika ya 16 na baadaye dakika ya 70.
Mnigeria
Victor Moses ambaye alitoka katika kipindi cha pili, naye alikuwa kati ya
waliotikiza nyavu za wageni wao kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London.
Bao
pekee la Kazan lilipatikana kwa mkwaju wa penalti kupitia Natcho baada ya
nahodha John Terry kuunawa mpira.
Katika mechi nyingine za Europa usiku wa kuamkia leo, Spurs ikiwa nyumbani ilijikuta ikilazimika kusawazisha mara mbili dhidi ya Basle ya Uswiss ili kupata sare ya mabao 2-2.
Pamoja na
kufanikiwa kupata sare hiyo, Spurs ilipata pigo kubwa baada ya kiungo wake
nyota, Gareth Bale alipoumia vibaya baada ya kukanywagwa na beki wa Basle.
Upande mwingine
Benfica iliionyesha kazi nyumbani baada ya kuikaribisha Newcastle ya England na
kuichapa kwa mabao 3-1.
Bao pekee
la Waingereza hao lilifungwa na Papis Cisse huku wenyeji wakionekana kuwa
hatari zaidi na wangekuwa makini wangeweza kuibuka na ushindi mkubwa zaidi ya
huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment