May 23, 2013


Hii ilikuwa mara ya mwisho Kili Stars ilipotembelea Ikulu baada ya kutwaa Kombe la Chalenji, mwaka juzi. Leo ni zamu ya Taifa Stars ambayo imepata nafasi ya kumuona, kuzungumza na kula chakula cha mchana na Rais Jakaya Kikwete


Kikosi cha timu ya soka ya taifa, Taifa Stars kimeitwa katika Ikulu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Jakaya Kikwete.

Kikwete amewaita Taifa Stars kwa ajili ya kuzungumza nao kama kuwapa morali kutokana na michezo miwili migumu dhidi ya Morocco na Ivory Coast  inayowakabili.


Mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu amethibitisha kuhusiana na Stars kupata mwaliko huo.

“Kweli leo tutakuwa nao hapa ikulu, lakini mambo mengi yatajulikana baadaye, hivyo mvute subira,” alisema Rweyemamu, mmoja wa waandishi mahiri wa mwanzo wa michezo nchini Tanzania.

Lakini Rais Kikwete atakula chakula cha mchana na kikosi cha Stars ambayo baadaye jioni itaendelea na mazoezi chini ya Kocha Kim Poulsea.

Muda mchache kuanzia sasa, Stars watawasili katika ‘mjengo’ huo wenye rangi nyeupe ‘full’, tayari kukutana na Rais Kikwete.

Jana Stars, walilamba mamilioni baada ya Kamati ya Saidia Stars Ishinde chini Mohammed Dewji kuwapa Sh milioni 30.

Stars itaondoka nchini Mei 26 kwenda Addis Ababa, Ethiopia ambako itacheza mechi ya kirafiki kabla ya kuondoka kwenda Casablanca ambako itacheza mechi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia Juni 8.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic